Pata taarifa kuu
MISRI

Rais Sisi ashinda muhula wa pili wa urais Misri

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amechaguliwa kwa muhula wa pili baada ya matokeo ya awali kuonesha kuwa ameshinda kwa asilimia 92 ya kura zote, wakati huu ni asilimia 40 tu ya kura zote.

Aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Misri, Abdel Fatah al-Sisi ambaye anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi wa mwaka huu.
Aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Misri, Abdel Fatah al-Sisi ambaye anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi wa mwaka huu. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Watu milioni 25 kati ya milioni 60 walioandikishwa kama wapigwa sawa na asilimia 41.5 walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa siku 3 ambao ulimalizika Jumatano ya wiki hiim gazeti moja nchini Misri limeripoti kuwa watu milioni 20 walimpigia kura al-Sisi.

Mpinzani wa Sisi, Moussa Mostafa Moussa ameelezwa kupata kura laki 7 na elfu 21.

Gazeti la The Akhbar el-Youm hata hivyo halikusema idadi kamili ya watu waliojitokeza lakini likasema Sisi ameshinda kwa kura milioni 21.4 na mpinzani wake Mostafa Moussa kwa kura 721, 000 ya kura zote bila kutaja pia kura zilizoharibika.

Kwa mujibu wa gazeti la Al-Ahram limesema kura milioni 23 zilikuwa ni kura halali, milioni 2 ziliharibika kwa wapigaji kuweka alama katika eneo ambalo halikuwa sahihi.

Mpinzani wa Sisi alikuwa mwanasiasa asiye na umaarufu Moussa ambaye yeye mwenyewe ni mfuasi mkubwa wa rais ambaye alijisajili siku moja kabla ya kufungwa kwa zoezi la usajili wagombea na kuepusha uchaguzi kuwa wa mgombea mmoja.

Moussa ameripotiwa kukubali matokeo usiku wa Jumatano akiwaambia waandishi wa habari kuwa alitarajia angalau kupata asilimia 10.

Wagombea wengine kwenye uchaguzi huu walijitoa, wengine kukosa sifa na baadhi yao kukamatwa kwa tuhuma za kuanza kampeni kabla ya muda uliopangwa pamoja na udanganyifu.

Sisi aliingia madarakani mwaka 2014 kwa kupata ushindi wa asilimia 96.9 idadi ambayo huenda na safari hii akaifikia.

Kuingia kwake madarakani kulitokana na mapinduzi ya kijeshi aliyoyaongoza ya kumng’oa madarakani, Mohamed Morsi ambaye anatumikia kifungo gerezani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.