Pata taarifa kuu
MISRI

Wananchi wa Misri wanapiga kura katika siku ya 2 ya uchaguzi

Wananchi wa Misri wanapiga kura katika siku ya pili ya uchaguzi mkuu wa urais, uchaguzi ambao rais wa sasa Abdel Fattah al-Sisi anatarajiwa kushinda kirahisi dhidi ya mgombea mwingine ambaye hajulikani sana.

Mpiga kura akichovya kidole kwenye wino baada ya kupiga kura kwenye mji wa Alexandrie, 27 Machi 2018.
Mpiga kura akichovya kidole kwenye wino baada ya kupiga kura kwenye mji wa Alexandrie, 27 Machi 2018. REUTERS/Mohamed Abd El Ghany
Matangazo ya kibiashara

Idadi ndogo ya wapifa kura imeshuhudiwa siku ya Jumanne katika vituo vingi vya kupigia kura wakati ambapo vituo vilifunguliwa maajira ya 9.00 kwa saa za Cairo.

Mamlaka nchini Misri zimekuwa zikitoa wito kwa raia kujitokeza kwa uwingi kushiriki kwenye uchaguzi huu wa siku tatu, wakitarajia pengine idadi kubwa ya watu itajitokeza licha ya kuonekana tayari kuna hitimisho la nani ataibuka mshindi.

Mgombea pekee anayeshindana na Sisi, Moussa Mostafa Moussa, yeye mwenyewe anadaiwa kuwa mfuasi mkubwa wa al-Sisi na hata kujitokeza kwake kuliibua maswali.

Wagombea wengine walijiondoa kabla ya kuidhinishwa na tume ya uchaguzi, wengine walitolewa na wengine kushikiliwa kwa tuhuma mbalimbali.

Sisi mkuu wa zamani wa majeshi ya Misri, alichaguliwa mwaka 2014 mwaka mmoja baada ya kumuondoa madarakani mtangulizi wake Mohamed Morsi.

Jeshi lilimuondoa madarakani Morsi kutokana na maandamano makubwa ya raia waliokuwa wanadai kiongozi huyo kuondoka madarakani wakipinga Sera zake za kiislamu.

Sisi ambaye wakati anaingia madarakani alikuwa na umaarufu mkubwa na kupendwa na wananchi, umaarufu wake ulishuka kutokana na hatua za ubanaji wa matumizi katika Serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.