rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afrika Kusini Jacob Zuma

Imechapishwa • Imehaririwa

Zuma kufikishwa mahakamani ndani ya wiki chache zijazo

media
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma. REUTERS / Siphiwe Sibeko

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma huenda akafikishwa mahakamani ndani ya wiki chache zijazo akikabiliwa na mashtaka ya rushwa, udanganyifu na utakatishaji fedha katika kesi inayohusu mkataba wa mabilioni ya fedha ya ununuzi wa zana za kijeshi uliofanyika mlongo mmoja uliopita.


Akinukuliwa mmoja wa watu waliokaribu kwenye kesi hiyo, anasema usikilizwaji wa kwanza huenda ukafanyika mjini Durban kuanzia April 6.

Waendesha mashtaka kwenye kesi hiyo wanadai kuwa Zuma alijipatia fedaha nyingi kutoka kwenye manunuzi ua ndege za kivita, viatu pamoja na zana nyingine zilizozalishwa na makampuni ya Ulaya ikiwemo ile ya Uingereza ya BAE System na ile ya Ufaransa Thales.

Ilitangazwa juma moja lililopita kuwa, Zuma ambaye alijiuzulu nafasi yake mwezi uliipita atakabiliwa na mashtaka kutokana na mkataba uliotiwa saini mwaka 1990.

hata hivyo msemaji wa kitengo maalumu cha kupambana na wizi Hawks amesema tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hizo bado haijapangwa.

Hangwani Mulaudzi amesema anatarajia jalada la kesi hiyo kukamilika ndani ya juma moja lijalo.

Zuma aliondoka madarakani kutokana na shinikizo kutoka ndani ya chama chake katika mfululizo wa kashfa za rushwa zilizokuwa zikimuandama.

Kiongozi huyo anatuhumiwa kunufaika na kiasi cha dola za Marekani laki 3 na elfu 45 katika mkataba wa mwaka 1990.

2009 waendesha mashtaka waliamua kufuta mashtaka ya rushwa dhidi yake miezi michache tu kabla ya kuwa rais.

Mwa uliopita mahakama ilitoa uamuzi kupinga kufutwa kwa mashtaka dhidi yake hatua iliyosababisha kufunguliwa upya kwa jalada la uchunguzi na hatimaye kushtakiwa.

Zuma atakabiliwa na kesi moja ya ubadhilifu, makosa mawili ya rushwa, kosa moja la utakatishaji fedha na makosa 12 yanayohusu udanganyifu.