Pata taarifa kuu
SIERRA LEONE-UCHAGUZI

Sierra Leone: Upinzani walalama kucheleweshwa kwa duru ya pili ya uchaguzi

Kinara wa upinzani nchini Sierra Leone Julius Maada Bio amemtuhumu rais anayemaliza muda wake Ernest Bai Koroma kwa kujaribu kuchelewesha kwa makusudi uchaguzi wa duru ya pili ulipangwa kufanyika Jumanne ya wiki hii kwa kwenda mahakamani kujaribu kukifanya chama tawala kibaki madarakani.

Wafuasi wa mgombea wa upinzani Julius Maada Bio wakizozana na polisi mjini Freetown, Machi 7, 2018.
Wafuasi wa mgombea wa upinzani Julius Maada Bio wakizozana na polisi mjini Freetown, Machi 7, 2018. REUTERS/Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Mahakama kuu ya nchi hiyo mwishoni mwa juma iliiagiza tume ya taifa ya uchaguzi kusitisha maandalizi ya kura hiyo hadi pale kesi ya malalamiko ya uchaguzi itakaposikilizwa, kesi ambayo iliwasilishwa na mawakili wenye uhusiano na chama tawala.

Bio ambaye alishinda duru ya kwanza katika uchaguzi wa Machi 7 kupitia chama cha Sierra Leone People's, atashindana na Samura Kamara ambaye ni mgombea anayeungwa mkono na rais Koroma na anawakilisha chama tawala cha All People's Congress.

“Njama za chama cha APC ziko wazi kabisa: hawataki kuona uchaguzi wa duru ya pili ukifanyika kwa sababu wanajua matokeo yake kwakuwa uma wa wananchi wa Sierra Leone hawatakichagua,” alisema Bio wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Bio amesema Koroma atalazimika kuwajibika kwa chochote kitakachotokea baadae, kuchelewa au kufutwa kwa uchaguzi kunakotengeneza hofu ya kusababisha machafuko nchini humo.

Chama tawala cha APC kinategemea wapiga kura wa kaskazini mwa nchi hiyo kwenye miji Temne na Limba wakati chama cha upinzani cha SLPP chenyewe kina umaarufu mkubwa kusini mwa nchi hiyo hasa kwenye jamii ya Mende.

Baadhi ya wagombea na wafuasi wao walitumia matamshi ya ukabila wakati wa kampeni ambapo polisi pamoja na waangalizi wa uchaguzi wameeleza wasiwasi wao kutokana na matamshi hayo.

Bio amemtaka Koroma kuruhusu uchaguzu wa duru ya pili kuendelea kama ulivyopangwa na kukubali matokeo, akiongeza kuwa rais Koroma huenda akaleta machafuko nchini humi ikiwa atashindwa kuondoka mamlakani mwisho wa muhula wake Machi 27.

Koroma amehudumu mihula yake miwili lakini alizisha taharuki mwaka jana wakati aliposema kuwa ataendelea kusalia kuwa kiongozi wa chama pale atakapoondoka madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.