Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Zambia: Mpinzani mkubwa wa rais Lungu akamatwa Lusaka

Waziri wa zamani wa Zambia na ambae ni mkosoaji mkubwa wa rais Edgar Lungu, amekamatwa Alhamisi ya wiki hii jijini Lusaka kwa tuhuma za kujipatia faida kupitia mtandao wa kihalifu.

Rais wa Zambia Edgar Lungu.
Rais wa Zambia Edgar Lungu. UN Photo/Manuel Elias
Matangazo ya kibiashara

Chishimba Kambwili, kwa siku za hivi karibuni ameibuka kuwa kinara na mkosoaji mkubwa wa Lungu ambaye anakosolewa kwa kuongoza nchi hiyo kiimla na kuwakamata wapinzani wake.

“Ameshtakiwa kwa makosa 37 ya kuwa na mali ambazo upatikanaji wake umetokana na uhalifu na makosa mawili ni kutumia mapungufu ya watu kujinufaisha,” amesema wakili wa Kambwili, Keith Mweemba.

Mweemba amesema kuwa Kambwili alizuiliwa na polisi na alitarajiwa kupelekwa mahakamani Ijumaa ya wiki hii.

Kambwili ambaye ni mbunge kutoka chama tawala cha Patriotic Front, ni waziri wazamani pia wa mambo ya nje na aliwahi kuhudumu kama waziri wa habari chini ya utawala wa rais Edgar Lungu.

Tangu wakati huo ametofautiana na rais Lungu na mara zote amekuwa akimtuhumu rais na Serikali yake kwa kuwa fisadi.

Hata hivyo rais Lungu ameendelea kukanusha kuwa anatengeneza utawala wa kiimla nchini Zambia huku akiwatuhumu wapinzani wake kwa kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa mwaka wa 2016.

Miongoni mwa wanasiasa ambao wameshuhudia manyanyaso ya vyombo vya usalama ni pamoja na kinara wa upinzani Hakainde Hichilema ambaye tangu kushindwa uchaguzi uliopita amekuwa akiandamwa na kesi ikiwemo kesi ya uhaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.