Pata taarifa kuu
SOMALIA

Somalia: Watu 14 wapoteza maisha katika shambulio la bomu Mogadishu

Watu 14 wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa siku ya Alhamisi wakati gari lilipolipuka nje ya hoteli moja maarufu ijini Mogadishu, Somalia.

Raia wakiwa wanaondoka kwenye eneo la shambulio mjini Mogadishu hivi karibuni
Raia wakiwa wanaondoka kwenye eneo la shambulio mjini Mogadishu hivi karibuni REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Kundi la Al-Qaeda lenye uhisiano na wapiganaji wa Al-Shabab nchini Somalia limekiri kuhusika kwenye shambulio la mbele ya hoteli ua Weheliya katikati mwa mji wa Mogadishu, kundi hilo likidai lililenga mkutano wa viongozi wa Serikali.

Msemaji wa Serikali amesema watu 14 walipoteza maisha kwenye eneo la tukio na kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka wakati huu vikosi vya uokoaji vikiendelea kutafuta miili zaidi.

"kulikuwa na mlipuko mkubwa na idadi ya watu waliokufa mpaka sasa ni 14 na wengine kadhaa wamejeruhiwa,: alisema Abdiazis Ali Ibrahim, msemaji wa wizara ya mambo ya ndani.

Watu walioshuhudiwa tukio hilo wanasema ulitokea kwenye mtaa wa Makkah al-Mukarama moja ya mitaa ambayo inashughuli nyingi kuunganisha na eneo la kati la mji wa Mogadishu.

Mji wa Mogadishu umekuwa ukilengwa na mashambulizi ya mara kwa mara yanayotekelezwa na kundi la Al-Shabab linalopigana kuiangusha Serkali ya Somalia inayotambuliwa kimataifa.

Hoteli ya Weheliya ilishambuliwa na wanagmabo wa Al-Shabab mwaka 2015.

Shambulio jingine baya kwenye mji huo lilikuwa ni mwezi Februari ambapo watu zaidi 38 walipoteza maisha mjini Mogadishu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.