Pata taarifa kuu
MALI

Waziri mkuu wa Mali afanya ziara ya kwanza kaskazini mwa nchi

Waziri mkuu wa Mali Soumeylou Boubeye Maiga amefanya ziara yake ya kwanza ya kihistoria kwenye eneo la kaskazini mwa nchi hiyo ambapo pia kituo chake kingine kinatarajiwa kuwa mji wa Kidal ambao bado unakaliwa na waasi.

Waziri mkuu mpya wa Mali Soumeylou Boubèye Maïga.
Waziri mkuu mpya wa Mali Soumeylou Boubèye Maïga. FAROUK BATICHE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Saa chache kabla ya ziara yake wanajeshi watano wa Ufaransa walijeruhiwa mjini Kidal wakati kambi yao ya jeshi iliposhambuliwa, imesema taarifa ya jeshi la Ufaransa jijini Paris ikieleza namna mji huo ulivyo na usalama mdogo.

Jumla ya wanajeshi elfu 4000 wa Ufaransa wamepelekwa nchini Mali kutekeleza operesheni Barkhane wakiwa sambamba na wanajeshi wengine wa kulinda amani wa umoja wa Mataifa wapatao elfu 12000 walioko chini ya tume ya MINUSMA.

Maiga alichaguliwa kwenye nafasi hiyo mwezi Desemba mwaka jana na kupewa jukumu la kuimarisha usalama wakati huu makundi ya wanajihadi yakiendesha mashambulizi kulenga vikosi vya Serikali na vile vya kigeni hatua inayozusha hofu kuhusu uchaguzi mkuu wa mwezi Julai mwaka huu.

Maiga aliwasili kwenye mji wa Tessalit kaskazini mwa Mali asubuhi ya Alhamisi na alitembelea mji wa Kidal majira ya mchana.

Hakuna afisa yeyote wa juu wa Serikali ya Bamako aliyewahi kutembelea eneo hilo tangu mwaka 2014 wakati kulipoibuka mapigano wakati wa ziara ya waziri mkuu Moussa Mara ziara iliyosababisha jeshi la Serikali kupoteza mamia ya wanajeshi.

Waasi ambao walianza kupigana na Serikali mwaka 2012 katika vita walivyoungwa mkono na makundi ya kijihadi, walitia saini mkataba wa amani mwaka 2015 lakini bado wamekuwa wagumu kuiunga mkono Serikali.

Maiga alitangaza Jumanne ya wiki hii kutembelea eneo hilo bila kufanya shambulio lolote kwa lengo la kuwasikiliza wananchi na kutambua shida zao.

Wazir mkuu Maiga pia alitarajiwa kutembelea mji wa Gao na Timbuktu miji mingine ya kaskazini ambayo imeshuhudia mapigano mara kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.