Pata taarifa kuu
FAO-WFP-EU-NJAA

UN, EU zaonya kuhusu usalama wa chakula duniani

Usalama wa chakula kwa watu zaidi ya milioni 124 duniani ulikuwa hatarini hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, hali iliyosababishwa na kuongezeka kwa mizozo na ukame, imesema taarifa ya umoja wa Mataifa na ile ya umoja wa Ulaya.

Uhaba wa mvua na ukame kumeathiri maeneo mengi ya kusini mwa Afrika - WFP
Uhaba wa mvua na ukame kumeathiri maeneo mengi ya kusini mwa Afrika - WFP Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hali mbaya zaidi ya chakula ilishuhudiwa mwaka 2017 kaskazini mwa nchi ya Nigeria, Somalia, Yemen na Sudan Kusini ambako zaidi ya watu milioni 32 hawakuwa na chakula na walihitaji msaada wa haraka, imeongexa taarifa ya pamoja ya EU na UN kuhusu hali ya chakula.

“Vita na majanga yanyohusiana na mabadiliko ya tabia nchi vilileta madhara makubwa na kusababisha hali ya njaa kuongezeka baada ya miaka kadhaa ya hali hiyo kudhibitiwa.” imeongeza ripoti hiyo.

Idadi ya watu milioni 124 ni asilimia 15 zaidi ya idadi kama hiyo kwa mwaka 2016.

Ripoti inasema kwa sasa maeneo mengi hayafikikia kuanzia barani Afrika, mashariki ya kati na sehemu za Asia Kusini ambako vita na hali tete ya usalama imesababisha kutokuwepo na usalama wa chakula.

Hata hivyo ukame uliokithiri kwenye nchi za pembe ya Afrika, mafuriko barani Asia na vimbunga kwenye nchi za America na visiwa vya Caribbean vyote hivi vilichangia kuenea kwa baada la njaa.

Kuelekea mbele ripoti hii imesema kuwa mizozo na usalama mdogo huenda vikasalia kuwa changamoto kwa usalama wa chakula mwaka 2018 na kuathiri nchi za Afghanistan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kaskazini mwa Nigeria na eneo la ukanda wa ziwa Chadi, Sudan Kusini, Yemen pamoja na Libya na eneo la kati la Sahel kwenye nchi za Mali na Niger.

Nchi ya Yemen itaendelea kuwa muhanga mkubwa wa baa la njaa na ukosefu wa chakula, imesema ripoti hii na kuongeza kuwa hali itazidi kuwa mbaya zaidi kwa kuwa maeneo mengi hayafikiki, kuporomoka kwa uchumi na milipuko ya magonjwa.

Athari za ukosefu wa mvua kwa mazao na uzalishaji wa wanyama kunatarajiwa kuendelea kushuhudiwa hasa kwenye maeneo ya wafugaji na wakulima nchini Somalia, Kusini mwa Ethiopia na mashariki mwa Kenyam Senegal, Chadi, Niger, Mali, Mauritania na Burkina Faso, imesema ripoti hii.

Hata hivyo ripoti hii imetabiri kuwa kusini mwa Afrika huenda hali ikawa nzuri zaidi mwaka huu kutokana na kushuka kwa bei ya chakula.

Ripoti hii iliwasilishwa na umoja wa Ulaya, shirika la mpango wa chakula duniani WFP na shirika la chakula na kilimo duniani FAO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.