rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Zimbabwe Robert Mugabe Emmerson Mnangagwa

Imechapishwa • Imehaririwa

UNDP kuisadia Zimbabwe kuelekea maandalizi ya Uchaguzi Julai

media
Raisi wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa REUTERS/Denis Balibouse

Umoja wa mataifa umetangaza kuunga mkono uchaguzi mpya unaoandaliwa kufanyika mwezi Julai nchini Zimbabwe na kuitaka serikali ya taifa hilo kutoa kipaumbele cha dharura kwa uchumi wa taifa hilo.


Achim Steiner, kiongozi wa mpango wa maendeleo katika umoja wa mataifa UNDP alikuwa ziarani jijini Harare na kukutana na raisi Emmerson Mnangagwa.

Steiner amesema Umoja wa mataifa unaendelea kuunga mkono mchakato wa maandalizi ya uchaguzi na jitihada za kuinua uchumi.

Uchaguzi wa uraisi unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi August ambapo Mnangagwa atakabiliwa na ushindani tangu alipochukua madaraka kutoka kwa aliyekuwa kiongozi mkongwe wa taifa hilo Robert Mugabe, ambaye alijiuzulu mwezi Novemba baada ya kutawala kwa takribani miongo minne.