Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-UPINZANI

Vyama vya UDPS, MLC na UNC kushiriki Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba

Vyama vitatu vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimetangaza kuwa vitashiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwishoni mwa mwaka huu bila ya kumtaja kiongozi aliye uhamishoni Moise Katumbi ambaye juma hili alitangaza nia yake ya kuwania urais.

Félix Tshisekedi,  kiongozi wa chama cha upinzani cha UDPS.
Félix Tshisekedi, kiongozi wa chama cha upinzani cha UDPS. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Vyama vya UDPS kinachoongozwa na Felix Tshisekedi na MLC cha Jean-Pierre Bemba na kile cha spika wa zamani Vital Kamerhe UNC vimethibitisha nia yao ya kushiriki uchaguzu wa Desemba 23 mwaka huu katika taarifa yao ya pamoja.

Viongozi hawa pia wameeleza kuguswa na hali duni ya usalama Mashariki mwa nchi hiyo pamoja na kutokuwa na imani na mitambo ya uchaguzi ya Kielektroniki wanayidai kuwa huenda ikawa imeshawekewa taarifa kukisaidia chama tawala.

Katika taarifa yao vyama hivi havikutaja popote jina la Katumbi wala kuonesha kuwa wamejiunga kwenye vuguvugu lake alilolizindua juma lililopita jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Katumbi ambaye ametangaza kuwa atarejea nyumbani hivi karibuni, ili kuanza mchakato wa kuwania urais mwezi Desemba mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.