rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Joseph Kabila Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu 30 wauawa mkoani Ituri baada ya mapigano ya kikabila

media
Wakimbi kutoka jimbo la Ituri baada ya kukimbia makwao kwa sababu ya vita vya kikabila JOHN WESSELS / AFP

Watu 30 wameuawa usiku wa kuamkia Jumanne katika mkoa wa Ituri, Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Mkuu wa Wilaya ya Bahema Kaskazini Willy Pilo Mulindro, amesema wamethibitisha vifo hivyo huku miili nyingine ikiokotwa msituni.

Hata hivyo, radio ya Umoja wa Mataifa, Radio Okapi,  inasema kuwa  watu walipoteza maisha ni 41.

Nyumba za watu katika Wilaya hiyo pia zinaripotiwa kuteketezwa moto huku wasiwasi ukiendelea kushuhudiwa.

Jamii ya makabila ya Hema na Lundu ambao ni wafugaji na wakulima, wamekuwa wakipigana kwa muda mrefu sasa kwa sababu ya ardhi.

Mapigano haya yamesababisha vifo vya watu 130 tangu mwezi Desemba mwaka uliopita kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Habari la Ufaransa la AFP.

Maelfu ya watu hasa wanawake na watoto wamelazimika kukimbilia nchini Uganda kutokana na makabiliano haya ya kikabila na kuhofia usalama wao.