Pata taarifa kuu
AFRIKA-TILLERSON-UGAIDI-MAREKANI

Tillerson atamatisha ziara yake Afrika, aahidi msaada wa Marekani

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amehitimisha ziara yake barani Afrika na kuahidi nchi yake kuendelea kuisaidia Chad na mataifa megine ya Afrika katika vita dhidi ya ugaidi.

Rex Tillerson, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani akiwa na mwenzake wa Chad  Chérif Mahamat Zène, jijini  Ndjamena nchini Chad, Machi 12 2018
Rex Tillerson, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani akiwa na mwenzake wa Chad Chérif Mahamat Zène, jijini Ndjamena nchini Chad, Machi 12 2018 REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Tillerson alitembelea nchi tano za ukanda wa Afrika Mashariki na Magharibi, lakini alilazimika kupunguza muda wa ziara yake katika kile kilichoelezwa na wizara ya mambo ya nje kuwa ni ratiba ngumu za kiongozi huyo.

Baada ya kutembelea nchi za Ethiopia, Djibouti na Kenya katika ziara iliyogubikwa na uamuzi wa rais Trump kukubali kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un, alilazimika kuibana ziara yake kwa kutembelea nchi ya Chadi na Nigeria kwa siku moja pekee.

Kabla ya kurejea jijini Washington, waziri Tillerson akiwa Nigeria aliahidi nchi yake kuisaidia kwa vifaa vya Kiintelijensia katika kuhakikisha wasichana zaidi ya 110 waliotekwa mwezi uliopita na wapiganaji wa Boko Haram wanapatikana.

Kiujumla waziri Tillerson ameendelea kusisitiza utayari wa nchi yake katika kuzisaidia nchi alizotembelea vifaa vya kijeshi na taarifa za kiintelijensia kukabiliana na ugaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.