rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC ICC Jean-Pierre Bemba

Imechapishwa • Imehaririwa

Germain Katanga na Jean-Pierre Bemba wapoteza rufaa

media
Germain Katanga kiongozi wa zamani wa waasi nchini DRC www.icc-cpi.int

Majaji wa rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC, wamesisitiza kuwa aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini DRC Germain Katanga, alipe fidia ya Dola Milioni 1 kwa waathiriwa wa mateso yaliyotekelezwa na waasi wake katika mkoa wa Ituri mwaka 2003.


Katanga aliyehukumiwa jela miaka 12 na kutozwa faini hiyo ambayo aliamua kukata rufaa akisema hana uwezo wa kulipa fedha hizo.

Hata hivyo, Majaji wametofautiana na Katanga na kumtaka kulipa fedha hizo wakisema hana sababu ya kuepuka hilo.

Waathiriwa 297 waliotambuliwa kuteswa na waasi hao hasa kubakwa kwa wanawake na wasichana katika kijiji cha Bogoro, watalipwa Dola 250 kila mmoja.

Wakati uo huo, Mahakama hiyo  imetupilia mbali rufaa ya aliyekuwa Makamu wa rais Jean-Pierre Bemba aliyepatikana na kosa la kuwahonga mashahidi 14 kusema uongo ili kumtetea wakati kesi yake ikiendelea.

Bemba amefungwa mwaka mmoja zaidi na kutozwa faini ya ya Euro 300,000 kwa kosa hilo, ukiachilia mbali kifungo cha miaka 18 jela alichohukimiwa mwaka 2016 baada ya kuongoza vikosi vyake vya MLC  kutekeleza uhalifu wa kivita nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.