Pata taarifa kuu
MAREKANI-AU-TILLERSON

Tillerson aanza ziara barani Afrika, akutana na uongozi wa AU

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ameanza ziara yake barani Afrika, akiwa kiongozi wa juu wa serikali ya rais Donald Trump kuzuru bara la Afrika tangu alipoingia madarakani mwaka 2017.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson (Kushoto) akiwa na Moussa Faki (Kulia) Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson (Kushoto) akiwa na Moussa Faki (Kulia) Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika twitter.com/AUC_MoussaFaki
Matangazo ya kibiashara

Tillerson ameanzia ziara yake katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia na na kukutana na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja huo Moussa Faki Mahamat.

Ni ziara inayokuja baada ya viongozi wa Afrika kukasirishwa na kauli ya rais Trump mwezi Januari alipoyafafanisha mataifa ya Afrika kama shimo la choo.

Wakati wa kikao hicho kilichodumu kwa zaidi ya saa moja, Mkuu wa Tume ya Afrika alimwambia Tillerson kuwa kauli hiyo ya Trump imeshapitwa na wakati kwa sababu aliandika barua ya kuisikitikia.

Tillerson na Faki wamejadiliana kuhusu ushirikiano wa Marekani na bara la Afrika kuhusu masuala ya usalama, biashara na kupambana dhidi ya ufisadi.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa mataifa ya Afrika kuungana kushinda ugaidi hasa Al Shabab nchini Somalia lakini pia kuyasaidia mataifa ya Afrika Magharibi kushinikiza Korea Kaskazini kuachana na mradi wake wa nyuklia.

Tillerson pia anazuru Djibouti, Kenya, Chad na Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.