Pata taarifa kuu
SIERRA LEON-UCHAGUZI-MATOKEO

Raia wa Sierra Leone wasubiri mshindi wa Uchaguzi wa urais

Wananchi wa Sierra Leon wanasubiri mshindi wa Uchaguzi wa urais, kura zikiendelea kuhesabiwa baada ya kutekeleza haki yako ya kidemokrasia siku ya Jumatano.

Raia wa Sierra Leone walivyopiga kura Machi 07 2018 kumchagua rais mpya
Raia wa Sierra Leone walivyopiga kura Machi 07 2018 kumchagua rais mpya REUTERS/Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Ushidani mkali ni kati ya mgombea wa chama tawala APC Samura Kamara ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya nje na Julius Maanda Bio mwanajeshi wa zamani ambaye anawania nafasi hiyo kwa mara ya pili kupitia chama cha upinzani cha SLPP.

Jumatano usiku Polisi walivamia Ofisi za chama kikuu cha upinzani jijini Freetiown kwa madai kuwa walikuwa wamepata taarifa ya upinzani kudukua matokeo.

Mgombea mkuu wa upinzani Julius Maanda Bio amethibitisha kutokea kwa uvamizi huo lakini polisi hawakufanikiwa kuingia ndani ya Ofisi hizo kwa sababu hawakuwa na kibali.

Kiongozi wa waangalizi kutoka nchi za Jumuiya ya Madola, na rais wa zamani wa Ghana John Mahama, alikwenda kujionea kilichokuwa kinafanyika na kusema madai hayo ni ya uongo.

Licha ya Polisi kuzingira majengo ya chama hicho cha upinzani, wameendelea kukusanya na kujumuisha matokeo ya urais kuyalinganisha na yale ya Tume ya Uchaguzi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Mohamed Conteh amewataka wananchi kuwa wavumilivu kwa sababu kumfahamu mshindi huenda kukachukua siku kadhaa.

Mshindi atamrithi rais Ernest Bai Koroma ambaye anaondoka madarakani baada ya kuongoza nchi hiyo tangu mwaka 2007.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.