Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-UGAIDI-UFARANSA

Watu wanane wakiwemo wanajeshi wawili wakamatwa Burkina Faso

Watu wanane wakiwemo wanajeshi wawili wamekamatwa nchini Burkina Faso wakituhumiwa kuhusika katika shambulizi la kigaidi wiki iliyopita katika Ubalozi wa Ufaransa na Makao makuu ya jeshi jijini Ouagadougou.

Eneo liloshambuliwa na magaidi wiki iliyopita  jijini Ouagadougou.
Eneo liloshambuliwa na magaidi wiki iliyopita jijini Ouagadougou. Ahmed Ouoba / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo lilisababisha vifo vya wanajeshi wanane na kuwajeruhi wengine.

Serikali nchini Burkina Faso inasema imewahoji zaidi ya watu 60 kabla ya kuwakamata watu hao.

Hata hivyo, maafisa wamesema hawezi kuthibitisha iwapo kundi la kijihadi la JNIM lilihusika katika shambulizi hilo kama ilivyodai.

Hata hivyo, maafisa wanasema kuna uwezekano kuwa raia wa kigeni walihusika katika mashambulizi hayo.

Imeripotiwa kuwa washambulizi hao walikuwa wanazungumza lugha ya Kiarabu na Bambara, inayozungumza Mali na Burkina Faso.

Majihadi hao walidai kutekeleza mashambulizi hayo baada ya wanajeshi wa Ufaransa kuwauwa viongozi wake Kaskazini mwa Mali hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.