Pata taarifa kuu
SIERRA LEON-UCHAGUZI-USALAMA

Wananchi Sierra Leone wapiga kura ulinzi ukiimarishwa

Uchaguzi mkuu nchini Sierra Leone unafanyika siku ya Jumatano ulinzi ukiwa ukiimarishwa na wapiga kura kuonekana wakiwa njia panda katika kufanya uamuzi wa kuchagua mgombea gani kutoka vyama viwili ambavyo vimekua vikitawala tangu nchi hiyo ipate Uhuru.

Mabango ya wagombea siasa nchini Sierra Leone
Mabango ya wagombea siasa nchini Sierra Leone LA Bagnetto
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wapiga kura Milioni tatu na Laki Moja wamejiandikisha kupiga kura na vituo vya kupigia vimefunguliwa kuanzia saa moja asubuhi saa za Afrika Magharibi, na vitafungwa saa 12 jioni.

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi,NEC, Bwana Mohamed Conteh amesema kuwa maandalizi yote ya uchaguzi yako tayari na amewata wapiga kura kujitokeza kwa wingi bila woga kwa sababu ulinzi umeimarishwa.

Aidha, ameongeza kuw Tume yake imejipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika misingi ya usalama, uwazi, uhuru, haki na kuaminika na tayari vifaa vyote vimesambazwa katika vituo vyote vya kupigia kura.

Katika Uchaguzi huu, rais Siera Leone Ernest Bai Koroma hagombei baada ya kuongoza nchi hiyo kwa mihula mitano mfululizo na hivyo mgombea Samura Kamara atapeperusha bendera ya chama tawala cha All Peoples Party, APC.

Nacho chama kikuu cha upinzani SLPP kimemsimamisha mgombea Julius Maada Wonie Bioambaye alishindwa na rais Koroma katika uchaguzi wa mwaka 2012.

Siera Leon inakwenda katika uchaguzi huo huku ikikabiliwa na uchumi duni ambao ulitetereka kati ya mwaka 2014 mpaka 2016 kufuatia nchi hiyo kukumbwa na ugonjwa wa Ebola.

Matokeo ya awali katika uchaguzi huo yataanza kutangazwa ndani ya saa 48 baada ya kufanyika uchaguzi huo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.