rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Mafuriko yameua watu kumi na nane Iran (idara ya hali ya Dharura)

ICC DRC

Imechapishwa • Imehaririwa

Mahakama ya ICC kuamua rufaa ya Germain Katanga

media
Germain Katanga kiongozi wa zamani wa waasi nchini DRC www.icc-cpi.int

Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC mjini Hague nchini Uholanzi, siku ya Alhamisi, wataamua rufaa iliyowasilishwa na Germain Katanga kiongozi wa zamani wa kundi la waasi la FRPI nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Mwaka 2014, Mahakama ya ICC ilimhukumu Katanga miaka 12 jela baada ya kumpata na makosa matano ikiwemo vita vya uhalifu na makosa mengine ya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo mauaji na ubakaji.

Katanga alipatikana na kosa la kutekeleza makosa hayo dhidi ya maelfu ya wakaazi wa kijiji cha Bogoro mwaka 2003 katika jimbo la Ituri.

Mwaka 2017, Mahakama ya ICC iliamua kuwa watu 300 walioathiriwa na mashambulizi ya waasi hao, kila mmoja atalipwa dola 250 kama fidia.

Katanga anasema Majaji kubadilisha uamuzi huo wa kulipa fidia waathiriwa hao, kwa sababu hana fedha zozote za kutoa malipo hayo.

Katanga anakitumia kifungo hicho nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.