rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC ADF Nalu MONUSCO

Imechapishwa • Imehaririwa

MONUSCO yaitaka DRC kuwachukulia hatua waliotekeleza mauaji ya Ituri

media
Wanajeshi wa kulinda amani Mashariki mwa DRC, MONUSCO. ©MONUSCO

Mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Leila Zerrougui amelaani mauaji yaliyotokea katika Wilaya Djugu katika jimbo la Ituri wiki iliyopita na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 30.


Mwakilishi huyo wa UN anasema ameguswa sana na mauaji hayo ambayo wengi waliopoteza maisha ni watoto na wanawake wasiokuwa na hatua.

Aidha, ametaka jeshi la DRC kuchunguza mauaji hayo na kuwachukulia hatua wale wote waliohusika.

Naye Gavana wa Jimbo la Ituri Jefferson Abdallah Penembaka amesema wanafanya jitihada kuhakikisha wahusika wa mauaji hayo wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Wakati uo huo watu 6 wameuawa katika eneo la Eringeti wilayani Beni, wengi wakikatwa kwa mapanga.

Kiongozi wa Mashirika ya kiraia katika Wilaya hiyo Gilbert Kambale, ameimbia RFI Kiswahili kuwa waliotekeleza mauaji hayo ni waasi wa ADF NALU.