Pata taarifa kuu
NIGERIA, NIGER, CAMEROON, CHAD-UN-USALAMA

Umoja wa Mataifa: Wakazi wa eneo la Ziwa Chad wanahitajia msaada wa haraka

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa zaidi ya watu Milioni 10 kutoka eneo la Ziwa Chad wanahitaji msaada wa kibinadamu. Umoja wa Mataifa unasema watu hao wanahitaji misaada hiyo kwa sababu wameathiriwa na ukosefu wa usalama katika mataifa yao.

Wakazi wa eneo la Ziwa Chad wameendelea kuathirika kutokana na mashambulizi ya Boko Haram.
Wakazi wa eneo la Ziwa Chad wameendelea kuathirika kutokana na mashambulizi ya Boko Haram. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa umetaka kutolewa msaada haraka iwezekanavyo ili kuwasaidia raia hao.

Hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulitoa taarifa ukizitaka taasizi za misaada ya kibinadamu kukusanya misaada zaidi ya kibinadamu na kifedha kwa ajili ya raia karibu Milioni 10 katika eneo la Ziwa Chad wanaohitaji misaada ya dharura. Kwa mujibu wa tangazo hilo la Umoja wa Mataifa, zaid iya dola Bilioni 1.5 zinahitajika ili kuwasaidia wakazi wa eneo hilo.

Mwaka uliopita zaidi ya dola Milioni 19 kuwasaidia raia Milioni tatu waliokua wakikabiliwa n ahali hiyo. Mwaka huu idadi hiyo imeongezeka na kufikia Milioni 10. Mpango wa Chakula Duniani (WFP) pia umeeleza wasiwasi wake juu ya uwezekano wa kutokea baa kubwa la njaa katika eneo hilo. Mbali na ukame, kundi la kigaidi a Boko Haram lina nafasi kuu katika kujitokeza hali hiyo ya mambo katika eneo la Ziwa Chad.

Wanamgambo wa Boko Haram wanazuia wanavijiji kuendesha shughuli zao za kilimo na  uvuvi katika eneo hilo. Jambo la kusikitisha ni kwamba kundi la Boko Haram linajidhaminia fedha kwa kuwapuuza matajiri na kuwalenga kwa mashambulizi raia maskini. Kundi hilo zaidi linatoza kodi kwa bidhaa, kupora vijiji na kuwateka nyara wanavijiji.

Nchi za eneo la Ziwa Chad zilizoathirika na mashambulizi na hujuma za magaidi wa Boko Haram ni Nigeria, Niger, Cameroon na Chad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.