Pata taarifa kuu
DRC-UN-UNHCR-USALAMA

UN yatahadharisha kuhusu maafa ya kibinadamu kusini mashariki mwa DRC

Vurugu zimeongezeka katika mkoa wa kusini mashariki mwa Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kuchochea "maafa ya kibinadamu ya kusikitisha," Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) limesema.

Raia wengi wa DRC wameyatoroka makazi yao katika maeneo mbalimbali ya mapigano.
Raia wengi wa DRC wameyatoroka makazi yao katika maeneo mbalimbali ya mapigano. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Katika mkoa huu umeendelea kukumbwa na machafuko ambayo yanaendelea kuongezeka tangu mwishoni mwa mwaka jana, huku makundi mapya ya watu wenye silaha yakiundwa bila kusahau ongezeko la idadi ya mashambulizi na matumizi ya silaha, amesema msemaji wa UNHCR Andrej Mahecic katika mkutano na waandishi wa habari.

"Leo tunatoa tahadhari: maafa ya kibinadamu kwa kiwango kikubwa yatatokea kusini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na mkoa wa Tanganyika unaendelea kukumbwa zaidi na vurugu, na kusababisha watu wengi kuyatoroka makazi yao visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu vikiendelea kuongezeka, "amesema.

Kwa zaidi ya miaka minne, kumekuwa na mapigano kati ya wanamgambo wanaowakilisha Waluba, kundi kutoka jamii ya Wabantu, na jamii ya Watwa. Mapigano haya yanasababishwa na kutokuepo na usawa kati ya wavinajiji kutoka jamii ya Wabantu ambao ni wakulima) na Watwa, ambao ni wawindaji wa kihistoria waliotengwa katika kupata ardhi na huduma za msingi.

Kwa mujibu wa Andrej Mahecic, vurugu hizi zakikabila tayari zimesababisha uhasama na watu wengi wameyatoroka makazi yao mkubwa wa idadi ya watu. Lakini tangu mapema mwezi Januari, kumekuwa na mapigano makali kati ya vikosi vya serikali vyaDRC na wanamgambo.

Katika majuma mawili ya kwanza ya mwezi Februari, mashirika yayanayoshirikiana na UNHCR yaliorodhesha matukio 800, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na ubakaji. Lakini vurugu nyingi zilifanyika katika maeneo ambayo ni vigumu kwa wafanyakazi wa kibinadamu kufika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.