Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SIASA-UCHUMI

Rais Jacob Zuma ajiuzulu

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma hatimaye alitangaza Jumatano usiku Februari 14 kujiuzulu, akisalimu amri baada ya chama chake kumtaka aachie ngazi.

ce mercredi 14 février.Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametangaza kujiuzulu kwake moja kwa moja kwenye televisheni Jumatano, Februari 14.
ce mercredi 14 février.Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametangaza kujiuzulu kwake moja kwa moja kwenye televisheni Jumatano, Februari 14. Phill Magakoe / AFP
Matangazo ya kibiashara

Chama cha African National Congress (ANC) kilikua kimetangaza kwamba kitawasilisha muswada wa kutokua na imani didi ya Rais Zuma leo Al hamisi ikiwa atakataa kujiuzulu kwa hiari yake.

Mapema siku ya Jumatano Rais Jacob Zuma alisema hakubaliani na uamuzi wa chama chake kumtaka ajiuzulu.

Zuma ambaye alizungumza na kituo cha taifa cha Televisheni cha SABC alisema, hatafanya kosa lolote na uongozi wa chama haujamwambia wanamtaka ajiuzulu kwa sababu gani, na hivyo anaonewa.

Kupitia hotuba yake iliyopeperushwa kwa njia ya televisheni Rais Zuma alisema anajiuzulu mara moja lakini akaongeza kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC.

Zuma mwenye umri wa miaka 75 amekuwa akikabiliwa na shinikizo za kumtakja ampe nafasi Makamu wake Cyril Ramaphosa, ambaye ndiye sasa kiongozi mpya wa chama.

Rais Jacob Zuma ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009, amekumbwa na shutuma nyingi za ufisadi, na hizo ndizo zimemponza na kuachia ngazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.