Pata taarifa kuu
MISRI-USALAMA

Misri : Wapiganaji 16 wa Kiislamu wameuawa Sinai

Wapiganaji 16 wa Kiiaislam wameuawa na watu 34 wamekamatwa katika operesheni kabambe ya vikosi vya usalama vya Misri iliyozinduliwa siku ya Ijumaa, kwa mujibu wa mamlaka za nchi hiyo.

Vikosi vya Misri vikiendesha operesheni kabambe dhidi ya wapiganaji wa Kiislam katika eneo la Sinai.
Vikosi vya Misri vikiendesha operesheni kabambe dhidi ya wapiganaji wa Kiislam katika eneo la Sinai. AFP
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hii inakuja ikiwa umesalia mwezi mmoja na nusu ya uchaguzi wa urais.

Maficho na ghala la silaha n amagari kadhaa vilivyokua vikitumiwa na wapiganaji hao vimeharibiwa katika mashambulizi ya anga yaliyoendeshwa katika eneo la Sinai, lakini pia katika Delta Nile na Jangwa la Magharibi, limesema jeshi katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumapili kwenye televisheni ya serikali.

Jeshi la anga, jeshila nchi kavu na lile la majini, bila kusahau polisi na kikosi cha ulinzi wa mipaka, walishiriki katika operesheni hiyo.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, ambaye alitangaza nia yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais mwezi ujao, aliamuru jeshi Novemba 29 kutokomeza wapiganaji wa Kiislamu ndani ya miezi mitatu, siku chache baada ya shambulio dhidi ya Muskiti, shambulio lililoua zaidi ya watu 300.

Wapiganaji wa Kiislamu wanaendesha mashambulizi yao mara kwa mara dhidi ya vikosi vya usalama tangu mwaka 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.