Pata taarifa kuu
AU-CHINA

Umoja wa Afrika wasema ni uongo kuwa China inaichunguza

Umoja wa Afrika unasema hauna siri inayoweza kuchunguzwa na taifa lolote, na kukanusha madai kuwa China imekuwa ikikusanya taarifa kwa siri na kuzituma mjini Shanghai.

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat (Kushoto) na Waziri wa Mambo ya nje wa China Wang Yi (Kulia) wakikutana jijini Beijing Februari 08 2018
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat (Kushoto) na Waziri wa Mambo ya nje wa China Wang Yi (Kulia) wakikutana jijini Beijing Februari 08 2018 REUTERS/Greg Baker/Pool
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya hivi karibuni iliyochapishwa katika Gazeti la Ufaransa la Le Monde, ilidai kuwa China ilificha mitambo katika jengo la Umoja wa Afrika ili kukusanya siri kuhusu shughuli za Umoja huo.

Gazeti la Le Monde, liliandika kuwa China ambayo imefadhili ujenzi wa jengo la Umoja wa Afrika, limedai kuwa Beijing imetega mitambo ya siri kunasa mawasiliano na kufuatilia mawasiliano yote katika Umoja huo.

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amesema madai ya Gazeti hilo ni ya uongo, kauli ambayo ameitoa alipokutana na Waziri wa Mambo ya nje wa China Wang Yi jijini Beijing.

“Sioni maslahi yoyote kwa China kuichunguza Umoja Afrika,” amesema Mahamat.

“Umoja wa Afrika haishughulikii masuala ya siri wala ya kujilinda, na sioni ni vipi China inaweza kutusaidia kujenga jengo hilo na kutuchunguza,” aliongeza.

Naye Waziri Wang amesema, hatua ya China kujenga jengo la makao makuu ya Umoja wa Afrika, ni katika kudumisha uhusiano kati ya nchi yake na mataifa ya Afrika.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.