rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Gambia Adama Barrow Jumuiya ya Madola

Imechapishwa • Imehaririwa

Gambia yarejea tena kwenye Jumuiya ya Madola

media
Balozi wa Gambia nchini Uingereza Francis Blain (Kushoto) akiwasilisha maombi kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Patricia Scotland jijini London thecommonwealth.org

Nchi ya Gambia imerejea tena kwenye Umoja wa nchi za Jumuiya ya  Madola, miaka mitano baada ya rais wa zamani Yahya Jammeh kuiondoa.


Jammeh ambaye aliondoka madarakani mwaka 2017, aliiondoa nchi hiyo baada ya kudai kuwa Jumuiya hiyo ilikuwa ya wakoloni.

Uanachama wa Gambia umekubaliwa tena katika Ofisi ya Jumuiya hiyo jijini London nchini Uingereza.

Baada ya kuingia madarakani,  rais wa sasa Adama Barrow, aliahidi kuirejesha nchi hiyo kwenye Jumuiya hiyo katika harakati za kuimarisha uhusiano wa nchi yake na mataifa ya nje.

Gambia inakuwa nchi ya nne kurejea kwenye Jumuiya hiyo baada ya Afrika Kusini, Pakistan na Fiji katika miaka ya hivi karibuni.

Jumuiya ya nchi za Madola iliundwa mwaka 1931 kwa lengo la kuziunganisha nchi zinazozungumza lugha ya Kiingereza.

Inaundwa na mataifa 52.

Kiongozi wa Jumuiya hiyo  ni Malkia wa Uingereza Bi.Elizabeth wa pili.