rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Nigeria Cameroon Vyombo vya Habari

Imechapishwa • Imehaririwa

Ahmed Abba atembelea makao makuu ya RFI na France 24

media
Ahmed Abba, mwandishi wa habari wa Idhaa ya Hausa ya RFI. © RFI-KISWAHILI

Ripota wa RFI idhaa ya Hausa Ahmed Abba amekuwa katika makao makuu ya RFI na FRANCE 24 jijini Paris nchini Ufaransa.


Abba, amekutana na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa kamati iliomuunga mkono wakati alipokuwa kizuizini.

Viongozi hao ni pamoja na katibu mkuu wa Francophonie, Michaelle Jean, Christophe Deloire (DELWARE) katibu mkuu wa shirika la wanahabari wasiokuw ana mipaka.

Abba aliachiwa huru mwezi Desemba mwaka jana baada ya kukaa jela katika kipindi cha miaka 2 kwa tuhuma za kuripoti taarifa kutoka kaskazini mwa Cameroun ambayo ilikuwa ni ngome ya kundi la wapiganaji wa Boko Haram.

Ahmed Abba amewashukuru wale wote waliosadia kuachiwa kwake.

“Kutokana na uungwaji mkono wa dunia nzima, uungwaji mkono wa RFI, uungwaji mkono wa mashirika yote ya haki za binadamu, niliendelea kuwa imara, haikuwa rahisi, lakini nilijikaza, mimi nimejitolea maisha, mimi na mwandishi na nitaendelea kuwahabarisha, kutafuta taarifa, nitafanya kazi na kuendelea kupambana kutafuta uhuru wa kujielekeza duniani, hatutarudi nyuma tutaendelea ili kukoa na kulinda taaluma yetu” amesema Abba.