rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Libya Ugaidi Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Shambulio la kigaidi laua watu 27 Libya

media
Mji wa Benghazi unaendelea kukumbwa na mashambulizi ya kigaidi. REUTERS/Stringer

Watu 27 wamepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa katika milipuko miwili iliyotokea karibu na msikiti mmoja katika mji wa Benghazi nchini Libya kufuatia shambulio la kigaidi.


Maafisa wa usalama wanasema washambuliaji walitumia gari lenye vilipuzi kutekeleza shambulio hilo.

Milipuko hiyo miwili ilitokea nje ya msikitiki karibu na eneo la Al Suleiman siku ya Jumanne jioni baada ya swala ya maghari wakati ambapo waumini walikua wakitoka ndani ya msikiti.

Mji wa Benghazi umekuwa kitovu cha machafuko kati ya wapiganaji na vikosi vya serikali.

Wanajeshi pamoja na raia ni miongoni mwa watu waliathiriwa na shambulizi hilo. Hata hivyo idadi ya watu waliojeruhiwa na vifo huenda ikapanda kutokana na watu wengi kujeruhiwa.

Haijafahamika ni kundi gani lililoshiriki katika shambulizi.

Libya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya mambomu,lakini milipuko hii miwili kutokea kwa muda wa dakika zisizozidi 20 ni jambo ambalo linawashangaza wengi nchini humo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya polisi washambuliaji walitumia magari mawili yaliyokua yamebebea vilipuzi. Gari lakwanza lililipuka wakati waumini walikua wakitoka ndani ya msikiti na gari la pili lililipuka muda mfupi dakika chache baadaye.

Machafuko nchini Libya yamesababisha vifo vya watu wengi, makundi ya kigaidi yakiendelea kunyooshewa kidole.