Pata taarifa kuu
SOMALIA-SIASA-MOGADISHU

Rais wa Somalia amfuta kazi Meya wa jiji la Mogadishu

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed amemfuta kazi Meya wa jiji la Mogadishu na kumteua Waziri wa Habari Abdirahman Omar Osman kushikilia nafasi hiyo.

Sehemu ya mji mkuu wa Somalia Mogadishu
Sehemu ya mji mkuu wa Somalia Mogadishu CC/Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Pindi tu baada ya uamuzi huo, usalama umeimarishwa zaidi jijini Mogadishu kwa hofu ya kutokea kwa utovu wa usalama.

Meya wa zamani Thabit Abdi Mohamed alihudumu kwa muda wa miezi tisa kabla ya kuondolewa katika nafasi hiyo.

Duru zinaeleza kwamba waziri mkuu wa nchi hiyo Hassan Ali Khairi ametofautiana na Meya wa Jiji Abdi Mohamed kuhusu kujitegemea lkwa mji mkuu pamoja na jimbo la Banadir.

Meya huyo aliyefutwa kazi Thabit Abdi Mohamed anaelezwa kuwa anaunga mkono Uhuru wa Mogadishu na Banadir na hivyo miji hiyo kuwa taifa la saba katika serikali ya shirikisho nchini Somalia itayokuwa na uhuru wa kujitawala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.