Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-MAANDAMANO-CENCO

Wasiwasi jijini Kinshasa kuelekea maandamano dhidi ya rais Kabila

Kuna hali ya wasiwasi jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuelekea maandamano yaliyoitishwa na Kanisa Katoliki katika miji yote ya nchi hiyo kumshinikiza rais Joseph Kabila kuondoka madarakani siku ya Jumapili.

Maandamano yaliyopita jijini Kinshasa dhidi ya rais Joseph Kabila
Maandamano yaliyopita jijini Kinshasa dhidi ya rais Joseph Kabila Reuters/ File
Matangazo ya kibiashara

Waandaji wa maandamano haya wanasema, yataendelea licha ya serikali ya Kinshasa kuyapiga marufuku.

Kuna wasiwasi kuwa kutatokea na makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa Polisi kama ilivyotokea mwisho mwa mwaka uliopita na kusababisha vifo vya waandamanaji saba na kuwajeruhi wengine.

Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO, limetoa wito kwa serikali kuruhusu kufanyika kwa maandamano hayo, kwa sababu ni haki ya kidemokrasia.

Aidha, MONUSCO imesema itatuma waangalizi wake kushuhudia namna maandamano hayo yatakayofanyika.

Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki CENCO, limetoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi na kuwaambia makasisi katika miji mbalimbali kusimamia maandamano hayo.

Uchaguzi nchini DRC ni Desemba mwaka huu, haijafahamika iwapo rais Kabila ambaye amekuwa akiongoza nchini hiyo tangu mwaka 2001, atawania tena.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.