rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Misri Ethiopia Abdel Fattah Al Sisi Hailemariam Desalegn

Imechapishwa • Imehaririwa

Misri na Ethiopia zasema hazitaki maji ya mto Nile kuharibu uhusiano wao

media
Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn akiwa na rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi jijini Addis Ababa Januari 18 2018 PHOTO | AFP

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wamesema hawataki mzozo wa matumizi ya maji ya mto Nile kuharibu uhusiano wa nchi hizo mbili.


Kauli hii ya kiongozi huyo wa Misri, ameitoa baada ya kuzuru jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kujadiliana na Waziri Mkuu Desalegn kuhusu ushirikiano wa nchi hizo mbili.

Aidha, viongozi hao wawili wamesema kuwa maji ya mto Nile yanastahili kuwaunganisha mataifa hayo kimaendeleo na watu wake na sio kuleta mzozo wa kisiasa.

“Tumekubaliana kuwa, mto huu mkubwa usiwe chanzo cha mgogoro kati ya nchi zetu, maji hawa yasitumiwe kama chanzo cha mzozo wa nchi hizo mbili,” alisema Hailemariam .

Licha ya hakikisho hili, mataifa haya yamekuwa yakivutana kuhusu matumizi ya maji ya mto Nile, hasa baada ya Ethiopia kuanzia mwaka 2012, kujenga bwawa kubwa la kuzalisha umeme barani Afrika, utakaozalisha megawatts 6,000.

Misri inakosoa mradi huo kwa kile inachosema  utasababisha maji ya mto huo kupungua na kuwaathiri raia wa Misri ambao wanategemea maji ya mto huo.