Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-USALAMA

Jeshi la Somalia lawaokoa watoto 32 walioajiriwa na Al Shabab

Jeshi la Somalia lilifanikiwa kuokoa watoto 32 waliokua wameajiriwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Al Shabab, baada ya kuendesh amashambulizi siku ya Alhamisi jioni katika shule inayomilikiwa na Al Shabab, serikali ya Somalia imetangaza leo Ijumaa.

Askari wa Somalia wakifanya ukaguzi katika magari, Mogadishu.
Askari wa Somalia wakifanya ukaguzi katika magari, Mogadishu. Getty Images/The Washington Post/Sudarsan Raghavan
Matangazo ya kibiashara

"Watoto 32 wa salama na serikali inawahudumia. Ni masikitiko makubwa kuona magaidi wanaajiri watoto. Hii inaonyesha jinsi gani hawana nguvu, wakati ambapoi wanaendelea kupoteza katika uwanja wa vita, huku raia wakifutilia mbali vitisho kutoka kundi hilo, "amesema Waziri wa Habari, wa Somalia, Abdirahman Omar Osman.

Al Shabaab imethibitisha kuwa shule, iliyoko mkoa wa Shabelle, ilishambuliwa na vikosi vya serikali, vikisaidiwa na ndege zisizo na rubani. watoto wanne na mwalimu mmoja waliuawa, kundi la Al Shaba limesem akatika taarifa yake.

"Waliteka nyara wanafunzi wengine waliosalia," amesema Abdiasis Abu Musab, msemaji wa kijeshi wa Al Shabab.

"Human Rights Watch inhusika na vifo vya wanafunzi hao na mwalimu wao kwa kuwa iliwanyooshea kidole," Bw Musab amesema .

Katika ripoti iliyochapishwa wiki hii, shirika hili la kimataifa la haki za binadamu lilisema kuwa tangu mwezi Septemba 2017, Al Shabab ilikikua ikiwaamuru viongozi wa vijiji na walimu wa shule za dini kuwakabidhi mamia ya watoto kutoka umri wa miaka nane.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.