Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Boko Haram yaua watu tisa Nigeria

Magaidi wa Boko Haram nchini Nigeria, wamewauwa watu tisa katika mashambulizi mawili yaliyotelezwa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Boko Haram imeendelea kulaumiwa kote duniani na hatua zimeanza kuchukuliwa dhidi yake.

Jeshi la Nigeria likiendelea kuwasaka wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Jeshi la Nigeria likiendelea kuwasaka wapiganaji wa kundi la Boko Haram. REUTERS/Tim Cocks
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa usalama wamethibitisha kutokea kwa mashambulizi hayo katika vijiji vya Jinene na Ngala katika jimbo la Borno.

Wapiganaji wa Boko Haram wamewauwa watu zaidi ya elfu kwa kipindi cha miaka tisa sasa, na wengine zaidi ya milioni mbili kukimbia makwao.

Nigeria imeendelea kukumbwa na mashambulizi ya Boko Haram, huku maefu ya raia wakilazimika kuyahama makazi yao.

Kundi hili limekua likijihusisha na mauaji na kuwateka nyara watu katika maeneo mbalimbali. Watu kadhaa wakiwemo wanafunzi wasichana wa chibok wanaendelewa kushikiliwa na kundi hili katika eneo lisilojulikana mpaka sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.