Watu wasiopungua 20 wauawa katika mapigano Libya
Mapigano makali yaliyozuka katika uwanja wa ndege jijini Tripoli jana kati ya waasi na jeshi la serikali, yamesababisha vifo vya watu 20. Ndege tano zimeathiriwa na mapigano hayo, kwa mujibu wa maafisa wa usalama.
Imechapishwa:
Serikali nchini Libya, inasema mapigano hayo yalianza baada ya waasi kujaribu kuvamia gereza moja wakiwa na lengo la kuwasadia wenzao kutoroka.
“Shambulio hilo ni jaribio la kundi moja la wapiganaji kuachiliwa kwa wafuasi wake waliokuwa wakishikiliwa na kundi wanalopingana nalo,” Serikali ya Libya inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa imesema.
Mapigano haya yaliyotokea yalihusisha makundi ya wanamgambo hasimu katika mji mkuu wa Libya, Tripoli
Haya ndio mapigano mabaya zaidi kuwahi kuripotiwa jijini Tripoli katika miezi ya hivi karibuni na kusabbaisba uwanja huo wa ndege wa kimataifa kufungwa.