Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Buhari aonya wanaochochea ghasia kati ya wakulima na wafugaji

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameonya kuchukuliwa hatua kwa wanaochochea mapigano kati ya wafugaji na wakulima nchini humo.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anataka ghasia kati ya wakulima na wafugaji zikomeshwe mara moja Nigeria.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anataka ghasia kati ya wakulima na wafugaji zikomeshwe mara moja Nigeria. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Onyo hili limekuja wiki moja baada ya watu 83 kupoteza katika mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika jimbo la Benue.

Mapigano haya ambayo yanahofiwa kuchochewa kisiasa yameanza tena kushuhudiwa nchini humo, kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Februari mwaka ujao.

Mapigano kati ya wafugaji wa jamii ya Fulani na wakulima yamekuwa yakiongezeka tangu mwaka ulipita yaani 2017 na huku maafisa wanasema mashambulizi bado yanaendelea.

Milipuko ya vurugu imekuwa ikitokea katika eneo la kati la Nigeria lakini mapigano hasa yamekuwa makali katika jimbo la Benue.

Mapigano makali ya mara kwa mara kati ya wafugaji wa kiislam kutoka jamii ya Fulani na wakulima wakristo yamekuwa yakitokea katika eneo hilo kwa muda lakini yalipamba moto zaidi mwanzoni mwa mwaka huu mpya.

Katika mwezi wa Novemba, Benue ilipitisha sheria ya kuzuia ufugaji horera, jambo ambalo ni kawaida kwa wafugaji wa ng’ombe kutoka jamii ya Fulani, pia kiliundwa kikosi chenye silaha kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo.

Ghasia na mauaji kati ya jamii za wafugaji na wakulima ni kitu kinachotokea mara kwa mara nchini Nigeria, hususan eneo la kati nchini humo ambako mapambano kuhusiana na malisho na haki ya kupata maji kati ya Wafulani, ambao ni wafugaji, na wakulima vimesababisha mauaji ya watu kadhaa katika miaka ya hivi karibuni. Hivi sasa yanaonekana kuchukua sura mpya ya ukabila na tofauti za dini. Rais Muhammadu Buhari amemuagiza mkuu wa Polisi kuhamia Benue ili kuidhibiti hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.