rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Joseph Kabila Siasa

Imechapishwa • Imehaririwa

Kanisa Katoliki lawaambia raia wa DRC wasichoke kutafuta haki ya kisiasa

media
Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC REUTERS/Thomas Mukoya

Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, linawataka raia wa nchi hiyo kutokata tamaa katika harakati za kutafuta haki ya kisiasa nchini humo, pamoja na kupigania haki zao.


Kauli hii imetolewa na Baraza la Maaskofu wa Kanisa hilo CENCO, ambao wana unashawishi mkubwa wa kisiasa nchini humo.

Msemaji wa CENCO Padri Donatien Nshole, amesema Kanisa halitanyamaza hadi pale haki ya kisiasa itakapopatikana.

Aidha, amesema kuwa Kanisa hilo halitishwa na yeyote.

Siku ya Ijumaa, kwa mara nyingine, Polisi jijini Kinshasa walitumia mabomu ya kutoa machozi na kufwatua risasi hewani, kuwatawanya waumini wa Kanisa hilo.

Waumini wa Kanisa pamoja na raia wengine walikuwa wamehudhuria ibada ya kuwakumba watu saba waliouawa mwisho wa mwaka 2017,  wakati wa maandamano ya kumshinikiza rais Joseph Kabila kuondoka madarakan.

Rais Kabila ambaye amekuwa rais tangu mwaka 2001, hajatangaza iwapo hatawania tena urais wakati wa Uchaguzi Mkuu mwisho wa mwaka huu, huku kukiwa na wasiwasi kuwa huenda akaamua kuonesha nia ya kuendelea kusalia madarakani.