rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC ADF Nalu Vyombo vya Habari

Imechapishwa • Imehaririwa

Hali ya sintofahamu yazuka Beni kufuatia kutekwa kwa Mkurugenzi wa RTGB

media
Katika msitu mkubwa wanakojificha waasi wa Uganda wa ADF, mashariki mwa DRC, jeshi la DRC (FARDC0 wakipiga doria. RFI/Sonia Rolley

Watetezi wa haki za Binadamu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanataka kuachiliwa huru kwa watu 10 akiwemo Mwanabari Jadot Mangwengwe, ambaye ni Mkurugenzi wa kituo cha redio RTGB.


Wanaminiwa kutekwa na waasi wa ADF Nalu mjini Beni siku ya Alhamisi Januari 11.

Watu hao walitekwa wakati wakirejea kutoka mjini Kasindi.

Miongoni mwa waliotekwa ni mkurugenzi wa radio washirika wa RFI, RTGB Beni ambayo huwa inajiunga na matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya RFI.

Kufuatia kutekwa nyara kwa Mangwengwe, viongozi wa radio zote katika mji na wilaya ya Beni, wameamua kusimamisha kazi kuanzia ijuma leo, hadi atakapopatikana mwandishi Jaddot Mangwengwe.

Mashuhuda wanasema watu hao walikuwa wamevalia sare za kijeshi ambapo baadae walitokemea na mateka wao kusikojulikana baada ya kuwapora kila walichokuwa nacho.

Makundi ya waasi wakiwemo Mai-Mai na kundi la ADF yamekuwa yakiyumbisha usalama kila uchao katika maeneo hayo kiasi kwamba hadi sasa ni vigumu kubaini wahusika.

 kundi la waasi wa Uganda linaloendesha harakati zake mashariki mwa DRC, limewaua mami ya watu katika maeneo mmbalimbali jirani na mji wa Beni.

Hivi karibuni jeshi la Uganda (UDF) likishirikiana na jeshi la DRC, (FARDC) liliendesha operesheni kabambe mashariki mwa DRC dhidi ya kundi hili.