Pata taarifa kuu
DRC-UN-SIASA

Antonio Guterres : Nina wasiwasi na kuahirishwa kwa uchaguzi DRC

Katika ripoti ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema ana wasiwasi baada ya uchaguzi mkuu kuahirishwa , kuna uwezekano wa kuahirishwa kwa uchaguzi huo kwa mara nyingine.

Antonio Guterres katika mkutano na waandishi wa habari New York, Septemba 23, 2017.
Antonio Guterres katika mkutano na waandishi wa habari New York, Septemba 23, 2017. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Antonio Guterres pia ameelezea masikitiko yake kwamba Uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23, 2018 unaweza kuahirishwa.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, hali ya kisiasa nchini DRC inaendelea kukabiliwa na "mgawanyiko mkubwa kwa wanasiasa na vyama vya kiraia", mgawanyiko uliojitokeza baada ya Tume ya Uchaguzi (Ceni) kutangaza kuahirisha kwa mara nyingine Uchaguzi mkuu ambao, kulingana na makubaliano ya kisiasa ya Desemba 31, 2016, "ungelifanyika mnamo Desemba 2017", amesem aBw Guterres.

Hata hivyo, kwa mujibu wa katibu mkuu, "serikali na chama tawala wanaonekana kuwa wako tayari kuheshimu kalenda ya uchaguzi."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.