rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Israeli AU Wahamiaji Benjamin Netanyahu

Imechapishwa • Imehaririwa

Netanyahu: Wahamiaji wa Kiafrika kufungwa jela ikiwa hawataondoka Israeli

media
Mmoja wa wahamiaji wa Kiafrika akiachiwa huru kutoka kituo cha Holot katika jangwa la Negev, Israeli. REUTERS / Amir Cohen

Serikali ya Israel imetangaza leo Jumatano nia yake ya kulipa dola 3,500 (sawa na euro 2,900) kwa wahamiaji kutoka Afrika wanaoishi kinyume cha sheria nchini humo ili kuwahimiza kuondoka Israeli ifikapo mwishoni mwa mwezi Machi, muda ambao watakabiliwa na kifungo ikiwa watakamtwa.


Wengi wa wahamiaji wa Afrika wanatoka Eritrea na Sudan. Wengi wanasema wamekimbia vita, matatizo mbalimbali ya kiuchumi na mateso, lakini Israeli inawachukulia kama wahamiaji "wa kiuchumi".

Mbali na kupewa kitita cha dola 3,500, wahamiaji watalipiwa nauli ya ndege kurudi nyumbani, au kuelekea "nchi nyingine". Nchi ambazo zimekubali kuwapokea ni Rwanda na Uganda, kulingana na mashirika ya haki za binadamu.

"Tumefukuza wahamiaji haramu 20,000 na sasa lengo letu ni kuwafukuza wengine," Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema katika kiako cha baraza la mawaziri katika kuidhinisha mpango huo.

Ameongeza kuwa kizuizi kilichojengwa kando ya mpaka na Misri kimezuia wakimbizi wengi kutoka Afrika. Ameelezea tatizo la usalama kwa Waisraeli wanaoishi katika vitongoji maskini kusini mwa Tel Aviv ambapo wahamiaji wengi kutoka Afrika wanaishi.

Kwa mujibu wa afisa wa uhamiaji ambaye hakutaka jina lake litajwe, wahamiaji 38,000 wanaishi kinyume cha sheria nchini Israel na zaidi ya 1,400 wanafungwa katika vituo viwili.

Wahamiaji, ambao baadhi yao wamekuwa wakiishi Israeli kwa miaka mingi, wana kazi lakini wanalipwa vibaya, kazi ambazo Waisraeli hawataki..

Benjamin Netanyahu amesema kuwa uwepo wa wahamiaji nchini Israel ni tishio kwa Waisrael.