Pata taarifa kuu
LIBERIA-UCHAGUZI-SIASA

George Weah achaguliwa kuwa rais wa Liberia kwa kishindo

Mwanasoka wa zamani wa Klabu za Ac Milan, Monaco, PSG, Manchester City na mshindi wa Tuzo ya Ballon d’Or 1995, George Weah, amechaguliwa kuwa Rais wa Liberia mara baada ya kushinda majimbo 12 kati ya 15 kwenye nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

George Weah ras mteule wa Liberia.
George Weah ras mteule wa Liberia. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa kupitia ukurasa wake wa Twitter amewashukuru watu wote waliompigia kura na wale ambao hawajampigia kura.

Weah amemshinda aliyekuwa Makamu wa Rais, Joseph Boakai mwenye umri wa miaka 75, ambaye amekuwa Makamu wa Rais kwa miaka 12, amepata kura katika majimbo mawaili tu.

Weah ameshinda uchaguzi huo ambao ulikuwa na ushindani mkali. Katika uchaguzi huo, Mwanamama Ellen Sirlif ambaye ni rais wa sasa hakugombea kutokana na matakwa ya katiba ya nchi hiyo ambayo inamzuia kugombea kiti hicho zaidi ya vipindi viwili.

Ellen aliingia Ikulu mwaka 2006, na sasa Weah, mchezaji bora wa dunia wa zamani ambae uchezaji wake ulitokana na mchango wake kwa Klabu yake ya zamani anatarajia kula kiapo kuongoza nchi hiyo.

Weah alisajiliwa Monaco AS na kocha wa sasa wa Arsean Fc, Arsene Wenge. Uchaguzi wa 2006 ulioumpa ushindi Ellen, Weah aligombea na aliungwa mkono na Wenger.

Huyu ndiye George Weah wa Liberia
George Tawlon Manneh Oppong Ousman Weah ni mwanakandanda mashuhuri duniani na mwanasiasa aliyegombea urais wa Liberia mwaka 2006.

Weah alizaliwa 1 Oktoba 1966 katika jiji la Monrovia na alikulia katika kitongoji cha watu wenye maisha duni cha Clara. Kabla ya kujiunga na soka la kulipwa, Weah alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Mawasiliano la Liberia kama fundi simu.

Kielimu, Weah ana Shahada ya Kwanza ya Uendeshaji Michezo toka Chuo Kikuu cha Parkwood, London, Uingereza. Mwaka 1999 alipata shahada ya Udaktari ya Heshima toka Chuo Kikuu cha A.M.E Zion nchini Liberia.

Mwaka 1995 Weah alipewa tuzo na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuwa Mwanasoka Bora Duniani. Yeye ni mwanasoka pekee toka Afrika aliyewahi kupewa tuzo hiyo.

Mwaka huo huo alichaguliwa pia kuwa Mwanasoka Bora Ulaya na Mwanasoka Bora Afrika.

Weah alianza safari yake ya soka katika timu ya Liberia ya Incincible Eleven na Tonnerre de Yaounde, ya Cameroon.
Baada ya hapo alikwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya mwaka 1988.

Alijiunga na timu ya Monaco ambapo aliiongoza kushinda kombe la Ufaransa mwaka 1991. Baadaye alijiunga na Paris Saint Germain mwaka 1992 hadi 1995.

Aliiongoza timu hii kuchukua kombe la ligi ya Ufaransa mwaka 1994. Mwaka 1995-2000 alikuwa akiichezea timu ya AC Milan ambayo ilishinda ligi ya Italia mwaka 1996 na 1999. Mwaka 2000 aliondoka AC Milan na kujiunga na Chelsea, baada ya muda mfupi alijiunga na Manchester City na baadaye Marseille mwaka 2001.

Alimaliza soka la kulipwa akiwa na timu ya Al Jazzira ya Falme ya Nchi za Kiarabu.

Weah amekuwa akitoa misaada kusaidia wananchi wa Liberia. Mwaka 2004 alipewa tuzo ya Arthur Ashe kwa juhudi zake za kusaidia kujenga nchi yake.

Kwa sasa Weah ameibuka mshindi wa kiti cha urais nchini Liberia ambaye sasa anasubiri kuapishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.