rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Cameroon Ufaransa

Imechapishwa • Imehaririwa

Mwandishi wa RFI Ahmed Abba ahukumiwa kifungo cha miezi 24 jela, hata hivyo kuwa huru

media
Ahmed Abba, Mwanahabari wa RFI Hausa www.rfi.fr

Mahakama ya kijeshi mjini Yaounde, Cameroon imemuhukumu kifungo cha miezi 24 jela mwanahabari wa RFI idhaa ya lugha ya Hausa Ahmed Abbakatika kesi ambayo alikuwa amekata rufaa.


Katika hukumu ya awali mahakama hiyo ilimuhukumu kifungo cha miaka 10 jela kwa tuhuma za kushirikiana na makundi ya kigaidi.

Hata hivyo mapema hivi leo mahakama hiyo ya kijeshi ilimfutia Abba mashtaka ya kujihusisha na makundi ya kigaidi na badala yake kumkuta na hatia ya kosa la kutofichua makundi hayo.

Hata hivyo kwa mujibu wa sheria Abba atakuwa huru kutokana na sehemu ya kifungo chake kuwa tayari amekitumikia akiwa jela wakati kesi yake ilipokuwa ikiendelea na toka alipokamatwa.

Kwa sasa Abba ametumia muda wa miezi 29 kifungoni ambapo alikamatwa Julai mwaka 2015 mjini Marouna kaskazini mwa nchi ya Cameroon ambako alikuwa ameenda kuripoti kuhusu kundi la Boko Haram.

Mamlaka nchini Cameroon zilikuwa zinamtuhumu Ahmed Abba kwa kushirikiana na kundi la Boko Haram kwa kubadilishana nao taarifa madai ambao mara zote Abba amekuwa akiyapinga mahakamani.

Mawakili wa Abba wameeleza kuridhishwa na uamuzi huu wa mahakama licha ya kuwa waliamini angeachiwa huru kwa kile walichosema mteja wao hakuwa na kesi ya kujibu.