Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-USALAMA

Askari wasiopungua 18 wa Somalia wauawa katika shambulio

Zaidi ya askari 18 wa Somalia wameangamia katika shambulio la kujitoa muhanga lilitokea leo Alhamisi katika chuo cha polisi mjini Mogadishu, nchini Somalia, kwa mujibu polisi.

Shambulio la kujitoa muhanga lagharimu maisha ya watu wengi Mogadishu, Somalia.
Shambulio la kujitoa muhanga lagharimu maisha ya watu wengi Mogadishu, Somalia. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Katika shambulio hilo askari kadhaa wamejeruhiwa na wengine wako katika hali mbaya.

"Mtu mmoja aliyevalia mkanda wa kulipuka aliingia katika kambi ambako kunapatikana chuo cha polisi, huku akijifananisha na ploisi na kujilipua," afisa wa polisi Mohamed Abdulle alisema, huku akibaini kwamba watu wengi wameuawa bila hata hivyo kutaja idadi.

Kwa mujibu wa mashahidi, polisi wamekua wamekusanyika kwa mazoezi yao ya asubuhi, wakati ambapo mshambuliaji alijilipua.

"Maafisa wa idara ya dharura wanaendelea na zoezi la uokoaji," amesema afisa wa polisi Abdulle.

Kambi iliyoshambuliwa ni sehemu ya shule kubwa ya polisi nchini Somalia.

Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo.

Kundi la Al Shabab, lenye mafungamano na al-Qaeda, limekua likitekeza mashambulizi dhidi ya vikosi vya polisi.

Shambulizi baya zaidi katika historia ya Somalia liligharimu maisha ya watu 512 mnamo Oktoba 14 wakati bomu lililotegwa katika lori bomu lililipuka mjini Mogadishu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.