Pata taarifa kuu
LIBYA-EU-WAHAMIAJI-USALAMA

Umoja wa Ulaya kuwarejesha makwao wahamiaji 15,000 kutoka Libya

Umoja wa Ulaya unatarajia kuwarudisha makwao wahamiaji 15,000 waliokwama nchini Libya hadi mwezi Februari 2018, Mkuu wa sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amesema leo alhamisi mjini Brussels, nchini Ubelgiji.

Wahamiaji haramu ambao wamekua wakijaribu kuingia Ulaya wakizuiliwa katika kituo kimoja cha Tajoura, Tripoli Mei 9, 2017.
Wahamiaji haramu ambao wamekua wakijaribu kuingia Ulaya wakizuiliwa katika kituo kimoja cha Tajoura, Tripoli Mei 9, 2017. MAHMUD TURKIA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hili ni lengo lililowekwa na kundi la wataalamu lililoundwa mwishoni mwa mwezi Novemba katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika mjini Abidjan, kwa kukabiliana na hasira iliyotokana na picha zilizorushwa na vyombo vya habari kuhusu kuepo kwa masoko ya watumwa nchini Libya.

Kundi hili linaundwa na Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, IOM (Shirika la Kimataifa la linalohusika na masuala ya wahamiaji) na shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR).

Kundi hili liliundwa kwa kukabiliana na hali mbaya ambayo inawakabili wahamiaji waliokwama nchini Libya, kutoka Afrika na Mashariki ya Kati, ambao wamekua wakijaribu kuingia Ulaya kwa kuvuka bahari ya Mediterranean.

Siku ya Jumanne, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International lilishutumu serikali za Ulaya kuwa kuhusika katika katika njia moja ama nyingne kwa kuzuiliwa kwa wahamiaji katikamazingira mabaya nchini Libya, ikizishtumu kuwasaidia vikosi vya ulinzi wa baharini nchini Libya, ambavyo vinahusika katika biashara haramu ya binadamu kwa mujibu wa shirika hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.