rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC MONUSCO UN

Imechapishwa • Imehaririwa

Askari kumi na wanne wa Monusco wauawa DRC

media
Askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa (Monusco) wakipiga doria katika mji wa Uvira Septemba 24, 2017. MONUSCO/Force

Askari kumi na wanne wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Monusco) waliuawa katika shambulizi la kuvizia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).


Katika shambulizi hilo askari zaidi ya arobaini walijeruhiwa, viongozi wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC wamesema leo Ijumaa.

Shambulizi lililolenga Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco) lilitokea siku ya Alhamisi usiku katika mkoa wa Kivu Kaskazini, unaopakana na Uganda na Rwanda.

Askari waliouawa ni kutoka Tanzania na askari 5 wa DRC (FARDC) pia waliuawa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa chanzo cha Umoja wa Mataifa nchini DRC.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaehusika na operesheni za kulinda amani, aliandika kwenye Twitter akithibitisha taarifa hiyo.

"Sala zetu tunazielekeza kwa familia na wenzetu wa Monusco, Kikosi cha usaidizi kimetumwa kwenye eneo la tukio na zoezi la kusafirisha waliojeruhiwa hospitalini linaendelea, Bw Lacroix ameandika kwenye Twitter leo Ijumaa.

Hali ya usalama mashariki mwa DR Congo inaendelea kutisha, zaidi ya watu 12,000 walikimbilia hivi karibuni nchini Zambia wakihofia kuuawa.