rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Etienne Tshisekedi Joseph Kabila

Imechapishwa • Imehaririwa

Chama cha upinzani cha UDPS chakumbwa na malumbani ya ndani

media
Bruno Tshibala amesema chama cha UDPS sio taasisi ya jadi ambayo mtoto anamrithi baba yake. JUNIOR KANNAH / AFP

Mvutano umeshika kasi katika chama cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo cha UDPS kuwania mrithi wa mwenyekiti wa chama hicho Etienne Tshisekedi aliefariki miezi kadhaa iliyopita.


Kwa muda wa siku tatu Waziri mkuu wa DR Congo Bruno Tshibala pamoja na wafuasi wa chama hicho walioungana naye wanakutana katika kongamano maalum kwa ajili ya kujiandalia uchaguzi.

Hata hivyo upande mwingine wa chama hicho unaoongozwa na Felix Tshisekedi umetupilai mbali kongamano hilo na kumuita Bruno Tshibala kuwa msaliti na alijiondowa mwenyewe katika chama hicho.

Akizungumza na RFI, Bruno Tshibala amesema hakuna aliemfukuza katika chama hicho na kwamba bado ni katibu mkuu wa UDPS na msemaji wa ressemblement.

Bruno Tshibala amesema chama cha UDPS sio taasisi ya jadi ambayo mtoto anamrithi baba yake.