Pata taarifa kuu
SENEGAL-HAKI

Mea wa Dakar kuachiwa huru wakati wowote

Hatimae Mea wa jiji la Dakar Khalifa Sall amekubali kutoa dhamana ili kuachiwa huru katika kesi inayo mkabili ya ubadhirifu wa mali ya umma, kesi ambayo inachukuliwa kuwa ya kisiasa.

Jela la Rebeuss ambako anafungwa  Meya wa Dakar Khalifa Sall.
Jela la Rebeuss ambako anafungwa Meya wa Dakar Khalifa Sall. G. thibault/RFI
Matangazo ya kibiashara

Kiwango cha dhamana, kina lingana na pesa ambayo inadaiwa kuwa ndio kiwango anachotuhumiwa kupitisha mlango wa nyuma.

Hata hivyo Khalifa Sall alikuwa amekataa kulipa dhamana, kabla ya kubadili msimamo baada ya ushawishi mkubwa wa watu wake wa karibu, familia na mawakili.

Wakili Koreisy Bah amesema lengo la dhamana hiyo ni kutaka aachiwe huru.

Hata hivyo upande wa Mahakama wanasema jumla ya kiwango kinachotakiwa kulipwa kikikamilika kiongozi huyo ataachiwa huru kwa dhamana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.