Pata taarifa kuu
EU-AU-USHIRIKIANO-UHAMIAJI-UTUMWA

Wahamiaji 3800 watakiwa kurejeshwa nyumbani kutoka Libya

Takriban wahamiaji 3,800 wa Kifrika walioko nchini Libya watarejeshwa nyumbani haraka iwezekanavyo. Kauli hii imetolewa leo Alhamisi na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU), Moussa Faki Mahamat, akibaini kwamba idadi ya jumla ya wahamiaji nchini Libya ni "kati ya 400,000 na 700,000."

Wavulana hawa, wahamiaji haramu, wamewekwa kizuizini Tripoli, mwezi Juni 2017.
Wavulana hawa, wahamiaji haramu, wamewekwa kizuizini Tripoli, mwezi Juni 2017. Florian Gaertner/Photothek via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, katika mkutano kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika, alitangaza siku ya Jumatano usiku kuanza hivi karibuni kwa "shughuli ya dharura ya kuondoa" wahamiaji wanaouzwa na makundi ya biashara ya binadamu nchini Libya.

 

"Wahamiaji 3800" walioorodheshwa katika kambi moja "wanataka kuondolewa mara moja katika nchi hiyo, na wanapaswa kurejeshwa haraka, amesema Moussa Faki Mahamat wakati wa mkutano huo wa 5 ambao unamalizika leo mjini Abidijan,nchini Cote d'Ivoire.

"Lakini si kambi moja tu," amesema, huku akibaini kwamba "serikali ya Libya ilituambia kwamba kuna kambi 42. Kwa kweli kuna zaidi ya hizo. Inakadiriwa wahamiaji 400 000 na 700 000 walioko nchini Libya. " "Ni lazima kwanza kuondoa kwa haraka wale ambao wako katika hali hali hiyo na tunatafakari kwa pamoja, Libya, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa, ili kupata ufumbuzi wa kudumu zaidi kwa suala la uhamiaji," Bw Mahamat alisema akihitimisha.

Mkutano kati ya Ulaya na Afrika umemalizika leo Alhamisi mjini Abidjan kwa kauli moja tu ambapo viongozi kutoka mabara yote wamekubaliana kupambana dhidi ya uhamiaji haramu na matokeo yake kama kama vile masoko ya watumwa nchini Libya. "Hatua ya kibinadamu inapaswa kuchukuliwa haraka" nchiniLibya, "mitandao haramu ya kusafirisha au kufanya biashara ya binadamu inapaswa kuvunjwa" na "Uchunguzi wa (kimataifa) unapaswa kufanywa," amesema Rais wa Cote d'Ivoire, Alassane Ouattara, wakati wa kuhitimisha mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.