Pata taarifa kuu
EU-AU-USHIRIKIANO

Mkutano kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika kuanza Abidjan

Mkutano wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika unatarajiwa kuzinduliwa leo Jumatano Novemba 29 katika mji mkuu wa Cote d'Ivoire, Abidjan. Viongozi 83 na washiriki 5,000 kutoka nchi 55 za Afrika na nchi 28 za Ulaya wanatarajiwa kwa mazungumzo ambapo masuala ya uhamiaji na usalama yatatawala mazungumzo hayo.

Mkutano kati ya EU-AU kuzinduliwa Abidjan tarehe 29 Novemba 2017.
Mkutano kati ya EU-AU kuzinduliwa Abidjan tarehe 29 Novemba 2017. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu, unaofanyika kila baada ya miaka mitatu, ni mfumo wa mashauriano ulioanzishwa kati ya Afrika na Ulaya.

Ilikuwa mwaka 2000 nchini Misri ambapo mazungumzo yalifanyika kwa mara ya kwanza katika ngazi ya bara ya Afrika na Ulaya. Na katika mji wa Lisbon mabara hayo mawili yalizindua mkakati wa pamoja wa Afrika na Ulaya. Tangu wakati huo, mikutano imekua ikifanyika kwa kasi na kufanyika kila baada ya miaka mitatu, barani Afrika, wakati mwingine barani Ulaya. Viongozi kutoka mabara haya mawili walikutana katika mji mkuu wa Libya Tripoli mwaka 2010, na mjini Brussels, nchini Ubelgiji mwaka 2014, kabla ya mkutano huu wa 5 mjini Abidjan.

Mijadala mikubwa imepangwa kufanyika kuhusu mada rasmi ya mkutano huo, ikiwa ni pamoja na uwekezaji katika vijana, lakini pia suala ambalo la wahamiaji, ambalo limekua tete baada ya visa vya kuuza wahamiaji kama watumwa kuripotiwa nchini Libya.

Kutokana na hali inayowakumba vijana wa Kiafrika (milioni 720 wenye umri wa chini ya miaka 25) wengi wamekua wakikata tamaa na namana ya kujimudu kimaisha na hivyo kuchukua uamuzi wa kukimbilia Ulaya au kuingia mitaani dhidi ya serikali zilizopo madarakani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika wanataka katika ushirikiano wao wa pamoja kutafutia ufumbuzi hali hiyo inayowakumba vijana. Wadadisi wanasema katika miaka 30 ijayo vijana watakua wamefikia bilioni 2.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.