Pata taarifa kuu
UFARANSA-AFRIKA-USHIRIKIANO

Rais wa Ufaransa kuzuru Afrika

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kuzuru barani Afrika wiki hii. Macron anatarajiwa kutembelea mataifa ya Burkina Faso, Cote d'Ivoire na Ghana.

Chuo Kikuu cha Ouagadougou, ambako rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiakuhutubia wanafunzi 88 kuhusu sera yake kwa Afrika.
Chuo Kikuu cha Ouagadougou, ambako rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiakuhutubia wanafunzi 88 kuhusu sera yake kwa Afrika. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa Afrika anatarajiwa kutumia ziara hiyo kujadiliana na viongozi wa mataifa hayo namna ya kuimarisha usalama na biashara kati ya Ufaransa na bara la Afrika.

Leo Jumatatu jioni Novemba 27 atakua Burkina Faso. Rais Macron atakuwa na mkutano wa kwanza na mwenzake Roch Marc Christian Kaboré.

Siku ya Jumanne asubuhi, atawahutubia wanafunzi 88 wa Chuo Kikuu cha Ouagadougu kuhusu sera yake kwa Afrika. Masuala ambayo anatarajia kuyapa kipaumbele ni pamoja na maendeleo ya sekta binafsi na elimu.

Lengo la ziara ya rais Macron ni kuimarisha ushirikiano kati ya Ufaransa na Afrika hasa vijana kutoka bara hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.