Pata taarifa kuu
Misri

Mamlaka nchini Misri zachunguza shambulizi lililoua watu 305 msikitini

Mamlaka nchini Misri zinachunguza shambulizi la Ijumaa katika msikiti huko rasi Sinai linalodhaniwa kutekelezwa na kundi la wanamgambo wa Islamic State ambapo jumla ya watu 305 wakiwemo watoto 27 waliuawa, shambulizi baya zaidi kushuhudiwa nchini humo hivi karibuni.

mwonekano wa eneo la tukio baada ya shambulizi ndani ya msikiti huko rasi Sinai Misri 25, Nov 2017.
mwonekano wa eneo la tukio baada ya shambulizi ndani ya msikiti huko rasi Sinai Misri 25, Nov 2017. . REUTERS/Mohamed Soliman
Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha jeshi la Misri hapo jana kishambulia maficho ya wanamgambo hao wanaodhaniwa ndio waliosababisha vifo hivyo katika eneo la rasi Sinai.

Mwendesha mashataka wa serikali amesema wanamgambo wapatao 30 wakipeperusha bango la kundi la Islamic State waliuzunguka msikiti Kaskazini mwa rasi Sinai na kufanya mauaji hayo wakati waumini wakiendelea na swala ya Ijumaa.

Hata hivyo kundi la Islamic State halikajiri kuhusika na shambulizi hilo, lakini ni washukiwa wakuu kwa kuwa msikiti huo unajihusisha na wafuasi wa Sufi tawi la waislam wa jamii ya Sunni ambao kundi hilo linawasema kuwa ni waasi.

Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi alitangaza siku tatu za maombolezo na kuaopa kujibu shambulizi hilo la kikatili kwa kutumia nguvu kali .

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.