Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-HAKI

UN: Tuna wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa ukiukaji wa haki za binadamu DRC

Idadi ya visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu wenye asili ya kisiasa - kunyimwa haki ya kuandamana, kukusanyika, kukamatwa kiholela vimeongezeka tangu mwanzoni mwa mwaka huu nchini DRC, kwa mujibu wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu.

Polisi wakitumwa katika mji wa Kinshasa.
Polisi wakitumwa katika mji wa Kinshasa. Eduardo Soteras / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla, visa vya ukiukwaji vimeongezeka kwa 60% kwa miezi miwili, Tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu imeelezea masikitiko yake. Visavya ukikwaji wa haki za binadamu vimeshuhudiwa nchini DRC kwa miezi mfululizo. Wanachama wa mashirika ya kiraia wanalengwa zaidi.

"Idadi ambayo tunayo kwa mwezi huu wa Oktoba inaleta tatizo kidogo. Hatuko kwenye njia sahihi, " Abdoul Aziz Thioye, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu amesema wakati akihojiwa na mwandishi wa RFI, Florence Morice.

Umoja wa Afrika (AU), Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO), Jumuiya ya nchi za Kanda ya Maziwa Makuu (ICGLR), Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wameomba serikali kutoa fedha zinazohitajika kwa ajili ya utaratibu wa uchaguzi.

Pia wameomba Tume ya Uchaguzi (CENI) kuheshimu kalenda ya uchaguzi, huku serikali ya DRC wakiiomba kuheshimu uhuru wa kufanya mikutano ya amani na kurihusu vyombo vya habari vya umma kutoa habari za uhakika biala sinikizo yoyote, kulingana na makubaliano ya Desemba 31, 2016. Tangazo hili lilitolewa baada ya mkutano kuhusu usalama wa kikanda uliofanyika siku ya Jumatano (Novemba 22) mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.